COMMENTS


Jumamosi, 4 Juni 2016

ANGELS (MALAIKA)




KUTEMBEA NA MALAIKA WA MUNGU
WALKING WITH THE ANGELS OF GOD


Angalizo
Tafadhali unaposoma kitini hiki jitahidi sana kufuata na kuomba kila ombi ambalo nimeliainisha ili kupata matokeo yaliyo bora zaidi
Usipige kopy kitini hiki ni vizuri ukakinunua kutoka kwa mwandishi kwa gharama yake ili Mungu akubariki.

Ezekiel 1
Nikaona, na tazama, upepo wa dhoruba ulitoka upande wa kaskazini, wingu kubwa sana, pamoja na moto, ukifanya duara ya nuru, na mwangaza pande zote, na katikati yake kitu kama rangi ya kaharabu, katikati ya moto huo. 5Kukatokea katikati yake mfano wa viumbe hai vinne. Kuonekana kwao kulikuwa hivi; walikuwa na sura ya mwanadamu. 6Na kila mmoja alikuwa na nyuso nne, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne. 7Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana. 8Nao walikuwa na mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao, pande zote nne; na wote wanne walikuwa na nyuso zao na mabawa yao hivi; 9mabawa yao yaliungana, hili na hili; nao hawakugeuka walipokwenda, walikwenda kila mmoja kuelekea mbele. 10Kwa habari za mfano wa nyuso zao; walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume; na hao wanne walikuwa na uso wa ng’ombe upande wa kushoto; na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia. 11Na nyuso zao na mabawa yao yalikuwa yametengana kwa juu; mabawa mawili ya kila mmoja yaliungana, hili na hili, na mawili yalifunika miili yao. 12Nao walikwenda kuelekea mbele, kila mmoja wao; roho ilikotaka kwenda ndiko walikokwenda; hawakugeuka walipokwenda. 13Kwa habari za kuonekana kwao vile viumbe hai; kuonekana kwao kulikuwa kama makaa ya moto yawakayo, kama kuonekana kwa vinga vya moto; moto ule ulikuwa ukienda juu na kushuka chini, katikati ya vile viumbe hai; na ule moto ulikuwa na mwangaza mwingi, na katika ule moto ulitoka umeme. 14Na vile viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme. 15Basi, nilipokuwa nikivitazama vile viumbe hai, tazama, gurudumu moja juu ya nchi, karibu na kila kimoja cha vile viumbe hai, pande zake zote nne. 16Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine. 17Yalipokwenda yalikwenda pande zote nne; hayakugeuka yalipokwenda. 18Katika habari za vivimbe vyake; vilikuwa virefu, vya kutisha; nayo yote manne, vivimbe vyake vimejaa macho pande zote. 19Na viumbe hao walipokwenda, magurudumu yalikwenda kandokando yao, na viumbe hao walipoinuliwa, magurudumu nayo yaliinuliwa. 20Kila mahali ambako roho hiyo ilitaka kwenda, walikwenda; walikuwa na roho ya kwenda huko; nayo magurudumu yaliinuliwa karibu nao; kwa maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu.21Walipokwenda hao, yalikwenda hayo nayo; na waliposimama hao, yalisimama hayo nayo; na walipoinuliwa hao juu ya nchi, magurudumu yaliinuliwa karibu nao; maana roho ya viumbe hai ilikuwa ndani ya magurudumu. 22Tena juu ya vichwa vya viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa anga, kama rangi ya bilauri, lenye kutisha, limetandwa juu ya vichwa vyao. 23Na chini ya anga mabawa yao yamenyoshwa, moja kulielekea la pili; kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande mmoja, na kila mmoja alikuwa na mawili yaliyowafunika miili yao upande wa pili. 24Nao walipokwenda nalisikia mshindo wa mabawa yao, kama mshindo wa maji makuu, kama sauti yake Mwenyezi, mshindo wa mvumo, kama mshindo wa jeshi; hapo waliposimama walishusha mabawa yao.25Tena palikuwa na sauti juu ya anga lile, lililokuwa juu ya vichwa vyao; hapo waliposimama walishusha mabawa yao. 26Na juu ya anga, lililokuwa juu ya vichwa vyao, palikuwa na mfano wa kiti cha enzi, kuonekana kwake kama yakuti samawi; na juu ya mfano huo wa kiti cha enzi, ulikuwako mfano kama kuonekana kwa mfano wa mwanadamu juu yake. 27Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, naliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote. 28Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nalianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.



Malaika ni halisi!! Mwaka 2007 nikiwa ninavuka barabara kuelekea shuleni,sikuwa nimeangalia vizur barabalani na gafla wakati ninavuka kumbe gari ilikuwa tayari Miguuni Pangu,namshukuru MUNGU kwakuwa kabla gari kabla  haijagonga miguu yangu nilirushwa kwa namna ya ajabu sana pembeni mwa barabara,halikuwa ni Jambo rahisi sana kwa akili ya kibinadamu,hii ilikuwa ni moja kati ya kazi za malaika katika maisha yangu
Ni mara nyingi sana nimekuwa nikiona MUNGU akituma malaika kwaajili yangu
Hebrew1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Malaika ni roho si watu wenye mwili kama sisi ni roho japo kuwa wanaweza kuvaa mwili kwa sababu ya kazi maalumu.
Malaika kwa kiriki ni Angelos ambayo ina maana ya wajumbE
Mwanzo 24:7
BWANA, MUNGUwa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko

Katika biblia unaweza ukaona kila mahali ambapo palikuwa na watu wa MUNGU au pana kusudi la MUNGU ni lazima palikuwa na udhihirisho wa kimalaika
Kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo kila mahali nimalaika, na kila mahali amabapo malaika walihusishwa kila kitu kilikwenda vizuri
Ibrahimu katika mistari ya hapo juu anasema malaika angemtangulia mtumishi wake kwenda kumtafutia mke isaka,kwa sababu ukiwa na malaika huwezi kukosea katika kuchagua,hii ni kusema kuwa ni muhmu sana hata katika mambo madogo kuwashirikisha malaika.
Kuna tatizo katika kanisa la leo si watu wengi wanaelewa umuhimu wa malaika katika maisha yao ya kawaida. YESU pamoja na kuwa alikuwa ni Mwana wa MUNGU kuna wakati alihitaji msaada wa malaika
Malko 1:13,
13Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.
luke 22:43
43Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Maisha ya YESU yalijaa miujiza kwa sababu iliwahusisha malaika katika kila kitu,alijua umuhimu wao. Tunaona mwanzo wa huduma ya YESU malaika wanaonekana wakimhudumia jangwani lakini pia mwisho wa huduma yake tunaona malaika pia wakimuhudumia
Si kwa sababu alikuwa ni MUNGU la hasha ni kwa sababu alijua sheria ya uumbaji ya kiungu imemuweka malaika kuwa mjumbe na muhudumu kwa watakatifu.
Hakuna jinsi unaweza ukafanikiwa katika maisha bila kuwahusisha viumbe hawa, ikiwa katika biashara au katika huduma malaika hufanya kazi kubwa katika kukuletea matunda.
MUNGU amewaweka kwa kusudi maalumu kwaajili yako.




UUMBWAJI WA MALAIKA NA MAUMBO YAO
Kwanza kabisa ni muimu kuelewa malaika wameumbwaje na wanafananaje kwa sababu kumekuwa na mkanganyiko mkubwa wa jinsi malaika wanavyofanana,wengine husema malaika wana mabawa na wako kama watu ,lakini ukweli ni kuwa si malaika wote wana mabawa na si malaika wote wanamaumbo kama binadamu,lakini kabla ya kuanza kuangalia jinsi wanavyofanana ni muhimu kuangalia Malaika wametoka wapi
UUMBWAJI WAO
MUNGU amewaumba malaika kwajili ya utumishi katika ufalme wake, maana yake wameumbwa kutumika katika kutekeleza majukumu ya ufalme waMUNGU
Malaika waliumbwa hata kabla ya mwanadamu kuumbwa maana yake ni kuwa wana muda mrefu kuliko uumbwaji wa mwanadamu,wanafahamu vile MUNGU alivyo muumba mtu na kwa sehemu wanafahamu thamani uliyonayo mbele za MUNGU
Ayubu 38:4
Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?
Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?
Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?
Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,
Na wana wote waMUNGU walipopiga kelele kwa furaha?


Ukiangalia mistari hiyo hapo juu utagundua ya kuwa MUNGU alipokuwa akiweka misingi ya dunia, malaika (wana waMUNGU) walikuwepo wakishangilia kwa furaha kuu.
Lakini pia tunapoangalia ya kuwa katika bustani ya edeni maandiko yanasema shetani alikuwepo tayar katika sura ya nyoka (maana yake tayar aliuwa ameshaumbwa na ameishi katika umalaika kwa kipindi na kisha akaanguka na kutupwa duniani)
Kimsingi malaika wamekuwapo hata kabla ya Adamu kuumbwa,pengine waliumbwa pamoja na ulimwengu wa kwanza,kabla ya Adamu.(angalia toleo jingine la kitabu kiitwacho Demonology)

MAUMBILE YAO
Malaika wana maumbo mbalimbali ambayo yanategemeana na makusudi ya uumbwaji wao,kuna malaika ambao wanafanana na magurudumu ya magari(ofanim) wengini wana sura ya wanadamu,kuna wenye mabawa na wasio na mabawa ,tutaangalia zaidi tutakapofika katika kipengele cha aina za malaika
Lengo langu hapa ni kuwa unahitaji kuwa na wigo mpana wa kimawazo juu ya maumbile yao kwa sababu unaweza ukawa umewaona na usitambue ya kuwa hawa ni malaika.






KAZI ZA MALAIKA
1.   Malaika huudumu katika Maombi kupeleka Maombi na kuleta majibu ya maombi.
Daniel 9:20-22,
Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za BWANA, MUNGU wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa MUNGU wangu; 21naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.22Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.

Wakati unapoomba MUNGU huwahusisha malaika katika kuhakikisha ya kuwa maombi yako yanamfikia MUNGU,lakini pia malaika huusishwa katika kuleta majibu ya maombi yako



Ombi: Baba katika Jina la YESU ninaomba achilia ulinzi wa Kimalaika katika maombi yangu kuanzia siku ya leo,katika jina la YESU napokea Amen


2.   Malaika  Huudumu katika kuleta ulinzi kwa Watu wa MUNGU
Daniel 6:21,
Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.22MUNGU wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Zaburi 34:7,
Malaika wa BWANA hufanya kituo,
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.




Ukiri: Ninakili na kutabiri ulinzi wa kimalaika usio wa kawaida  katika Maisha yangu



3.   Malaika huudumu katika kuleta mavuno

Ufunuo 14:18

Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. 18Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana. 19Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya MUNGU
Tumetumwa na MUNGU katika kuvuna nafsi za watu,kazi hii si rahisi kwa akili zetu wenyewe,MUNGU tayar anao malaika ili kukusaidia kuvuna hizo nafsi.wahusishe malaika katika mavuno
Wakati mwingine unaweza ukawa ni wakati wako wa mavuno(Baraka) nap engine inachelewa,mwite malaika wa mavuno akakuvunie na kukuletea


ombi: baba katika jina la YESU agiza malaika kwaajili ya mavuno yangu yaliyotayari,kwaajli ya Baraka zangu zilizo tayar katika jina la YESU napokea. Amen.

4.   Malaika huudumu katika kuleta ufunuo(revelation)na ufahamu(Knowledge)
Luke 2:47,
Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.

Daniel 8:16-19
Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya. 17Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.18Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima.19Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa.

Ufahamu juu ya neno la MUNGU na juu ya mambo yatakayo kuja badae,ufahamu juu ya Mambo tu ya kila siku ya kawaida.
Wakati mwengine unaweza ukajikuta unashindwa kufanya kitu sio tu kwa sababu hujui jinsi ya kufanya isipokuwa unaweza ukawa umekosa ufunuo juu ya hilo jambo
Wakati mmoja nikiwa ninaomba kwaajili ya Mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zilikuwa zimepita wakati ninaomba nikasikia neno la Hekima(ufunuo juu ya jinsi ya kukabiliana na Tatizo) ya kuwa nitamke neno la kinabii juu ya huyo mama nikilenga muda na jinsia ya mtoto atakaye jifungua.nikafanya hivo,na kwa ajabu ya MUNGU siku hiyo hiyo saa nane usiku akajifungua mtoto wa kiume sawa sawa na ufunuo ulioletwa na malaika.
Unapotembea na malaika wa ufunuo mambo mengi yanakuwa rahisi sana kukabiliana nayo.

Ombi: baba katika jina la YESU tuma malaika wako wa Ufunuo ili kunipa ufunuo wa mambo yaliyo magumu kwangu.katika jina la YESU napokea Amen



5.   Malaika huudumu katika kukupigania
Hii ni kazi nyingine ya malaika,kukuhudumia katika mapigano yako,malaika wanajua mbinu za kutwanga adui mpaka akimbie
Ufunuo 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa MUNGU wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za MUNGU wetu, mchana na usiku. 11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
Unahitaj malaika waingilie kati vita yako
Malaika wanauwezo wa kukupigania,kukushindia na kuwaadabisha adui zako
MUNGU anasema “nitawafanya adui zako kuja kwa njia moja na kuondoka kwa njia saba” tena anasema nitawaondoa adui zako ili wewe uweze kutawala.





Unabii: ninatabiri katika maisha yako,kila adui anayekuzuia hatima yako ising’are akamate moto sasa kwa jina la YESU,MUNGU awatawanye adui zako na kuchafua lugha zao Katika jina La YESU pokea.

6.   Malaika hukutangulia ili Kusawazisha njia
Kutoka 23:20
20Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.21Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 22Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. 24Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.
Zaburi 91:11
11  Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.


Hii ni kazi nyingine ya malaika,wanasafisha njia kwaajili yako ili wewe usijikwae katika lolote
Zaburi 91:11
11  Kwa kuwa atakuagizia malaika zake
Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

Wewe ni mtoto wa mfalme umezaliwa katika familia ya kifalme iliyojuu sana ,lakini pia wewe ni mfalme
ufunuo 5:10,
ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa MUNGU wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Mfalme anapopita mahali utaona njia inavyosafishwa,unakumbuka wakati raisi wa mareka Barrack Obama alipotembelea Tanzania,watu walideki hadi barabara,hiyo ndiyo hadhi ya mfalme,,lakini ona wewe ni zaidi ya Obama,ni mfale na pia ni Kuhani na kama haitoshi nimmiliki halali wa ulimwengu huu,ni mtoto wa mfalme aliye juu sana muumbaji wa kila kitu kinachokwenda chenye pumzi na uhai ,Yeye ndiye Bwana wa roho zote,Unahitaji malaika kukuandalia mazingira sit u ya Kiroho bali na ya kimwili pia,malaika wanaweza kushughulikia hata vitu vidogo sana ambavyo ww unavidharau
Siku moja mimi na Rafiki yangu tulikuwa tumtoka Chuoni tukiwa tumechoka sana na tukafika tu ndani na kulala,tulisahau kuzima taa na kufunga milango,ajabu usiku mwenzangua aliamka na kukuta taa zimezimwa,mlango umefungwa vizur kwa ndani na pia tumefunikwa mashuka,malaika waliaandaa usingizi wetu


Ukiri: ninakili uwepo wa malaika katika maisha yangu,kuandaa njia yangu na kusawazisha mahali nitakapo pita katika jina la YESU



7.   Malaika huudumu katika kukuletea mahitaji yako ya kimwili
1falme 19:5
Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 8Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa MUNGU.
Umewahi kusikia pesa za miujiza?,kazi za kimiujiza,mikataba na tenda za kimiujiza? Chakula cha kimiujiza, hiini kazi ya malaika wa mahitaji,unaporuhusu awe sehemu ya maisha yako unafungua mlango wa kushangazwa kila siku na miujiza isiyo na kokomo ya kila siku



Ombi: Baba katika jina la YESU ninaomba achilia malaika wako kwaajili ya miujiza yangu katika jina la YESU napokea Amen

8.   Malaika hutia Nguvu za Kusonga Mbele
Luka 22:42
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ 43Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.44Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Kuna wakati mwengine mambo hua magumu sana kiasi kwamba unaweza ukakata tama katika imani,ni kama YESU alifika mahali akakata tama juu ya ile changamoto ya msalaba mbele yake,akaomba na malaika akamtia Nguvu ili asonge mbele
Unapitia wapi, kumbukaMUNGU hakutuahidi kuwa angezuia majaribu yasitupate ila alisema,ujapopita katika moto hautakugharikisha,
Unajua unapoalika malaika njia yako huwa rahisi,hukuinua na kukutia moyo,wakati watu wengine wamekukimbia Roho wa Neema huwatuma malaika kukutia nguvu na kuwa marafiki wa Karibu sana Kwako.
Ombi: Baba katika Jina la YESU katika hili ninalopitia ninahitaji malaika kupita name katika jina la YESU Napokea amen

9.   Malaika huudumu uponyaji
Kuna malaika spesho kwaajili ya uponyaji wako,maraika Raphael ni malaika mkuu katika mambo ya uponyaji na opereshen mbalimbali,
Yeye huusika kurejesha afya na kuweka uumbaji wa MUNGU katika ukamilifu wake,hurejesha viungo,hufanya vipofu kuona na viziwi kusikia,ni malaika kwaajili ya maisha ya afya ya mwanadamu

10.               Malaika huuwa(they Kill)
Pamoja na kuwa malaika hufanya kazi njema kwaajili yetu,ni kweli pia kwa wale ambao wanachezea maisha yako na kuwa kwazo mbele yako MUNGU hutuma malaika kuwaondoa kabisa,wawe ni mapepo au watu.
1 samwel 2:6
Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
Unabii:ninatabili uwepo wa kimalaika katika maisha yako,kuuwa kila kitu kinachozuia usiingie katika kanani yako,kila kitu kinachozuia usiingie katika hatima yako iliyoboreshwa,kila kitu kinacho na kitakachozuia usiingie mbinguni,shoka limekwisha kuwekwa shinani ,pokea kwa jina la YESU.

11.               Malaika hukusindikiza kuingia katika Uzima wa milele (mbinguni)
2 falme 2:11
11Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.

2kor 2:2
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; MUNGU ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; MUNGU ajua); 4ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene
Unapolala katika Bwana au unapochukuliwa kimaono ni malaika ndio watakuongoza kufika kule unakotarajia kufika.

Basi sasa tumeona baadhi tu ya kazi za kimalaika katika maisha yetu ni nyingi sana kiasi kwambu tukianza kutaja zinaweza kutuchukua wiki nzima kuelezea,hivo basi tuangalie aina za Malaika

AINA ZA MALAIKA
Kuna aina nyingi sana za malaika lakini nitajaribu kutaja baadhi yake tu
Ikumbukwe kuwa malaika wana fanya kazi katika mpango maalumu wana vyeo na ngazi za kimadaraka yafuatayo ni baadhi ya makundi ya malaika


1.   MALAIKA WAKUU
Hawa ni malaika maalumu na hutumwa kwa kazi maalumu,hawatumwi hovyohovyo(the heavenly special force) na wanapotokea jua kuna ishu nzito,na kama ni mapepo yatapata shida ni labda yafe au yaongozwe sala ya toba(mapepo hayawezi kuongozwa sala ya toba)
Malaika mmoja anauwezo wa kufanya kazi za malaika elfu na elfu,hawa ndio malaika wakuu na Jumla yao wako saba
1.   YURIEL(NURU YA MUNGU)
Huyu ni malaika ambaye anahusika sana na uangalizi wa Dunia na mahali maalumu palipowekwa kwaajili ya mateso na vifungo (Tartarus),lakini pia kulinda heshima ya Jina la Bwana wa Majeshi,kwa wale wanao tukana Jina la Bwana huyu malaika na kikosi chake ndio kazi yao kuwashughulikia,wanaotukana wokovu wako na kukuona kinyaa kwa sababu unamtumikia MUNGU watakutana na Huyu jamaa
Wengi wa watumishi wa MUNGU hulindwa na malaika huyu kwa sababu maandiko yanasema watumishi wa Bwana wamebeba Jina la Bwana.
Huyu ni malaika ambaye ni hatari sana,huwa anaua kabisa,au kukuabisha kabisa ndio maana maandiko yanasema
isaya 54:17
17Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Unaweza ukaona kile kilichofanyika kwa kina Hauni na Miriam katika hesabu 12

2.   RAPHAEL (MUNGU mponyaji)
Huyu ni malaika aliyewekwa kwaajili ya roho za wanadamu,na uponyaji wa kila aina ya Magojwa,urejeshaji wa viungo na uhai,hufanya kazi kuhakikisha lile neno la uponyaji linakuwa halisi katika maisha yako,na unafurahia uzima wako(maandiko ya uponyaji)
3.   PHANUEL(uso wa MUNGU)
Huyu ni malaika anayehusika na Toba kwa wale wanaourithi wokovu,huusika katika kuleta majuto juu ya dhambi ili kupata toba ya Kweli na mwisho ondoleo la Dhambi.

4.   MIKAEL (nani kama Bwana)
Huyu ni malaika anaye husika katika katika maeneo makuu ya mwanadam kama uhai,lakini pia ni malaika anayehusika sana na vita na vurugu zinazosababishwa na mapepo
Ni malaika mwenye nguvu sana na anauwezo mkubwa sana wa kivita,Tunaona mara nyingi MUNGU humtumia huyu malaika katika mapambano,unaweza kuona matendo yake hapa
Ufunuo 12:7
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;8nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.9Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa MUNGU wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za MUNGU wetu, mchana na usiku.
Yuda 1:9
Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.


5.   GABRIEL(MUNGU ni nguvu zangu)
Huyu ni malaika wa habari njema, Ndiye malaika anyetumiwa sana kuleta ufunuo na ufahamu wa mambo ya Kiroho lakini pia ni malaika ambaye MUNGU amemuweka kwaa jili ya Paradiso na uangalizi wa Kundi jingine la Malaika linaloitwa makerubi
Luka 1:19
19Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za MUNGU; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema
Daniel 8:16
16Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya. 17Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.

6.   REMIEL
Huyu ni malaika kwaajili ya Ukuu,kwa wale ambao wanahitaji kufika mahali pa juu,katika biashara,katika Masomo katika kila kitu
7.   JOPHIEL
Huyu ni malaika wa hekima na maarifa.Ni mmoja kati ya malaika wakuu ambae yuko maarumu katika kuleta neno la ufunuo neno la maarifa.


KUNDI LA PILI LA MALAIKA
MAKERUBI (wenye uhai wane)
Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma. 7Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye. 8Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana MUNGU Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. 9Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi utukufu, na heshima, na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele,
Hawa ni malaika ambao wana sura nne
I.             Sura ya Ng’ombe – roho ya utayar,na Utumishi
II.           Sura ya Tai- uwezo wa Kuona vitu kutoka Mbali(prophetic eyes)
III.          Sura ya Simba- Ujasiri na Nguvu
IV.         Sura ya mwanadamu- upendo,utu na utashi
Malaika hawa kazi yao ni kulinda kiti cha MUNGU,aina hii ya malaika ndio waliotumwa na MUNGU kuilinda ile njia ya mti wa uzima katika bustani ya Edeni mwanzo 3:24
Lakini pia hawa ni malaika ambao MUNGU alimwamuru musa kutengeneza mfano wao ili kutitia kiti cha Rehema katika mahali patakatifu pa patakatifu na juu ya sanduku la agano. Angalia mfano hapo chini


KUNDI LA TATU
OPHANIM
Jina ophanim ni jina linalobeba maana ya wajumbe wenye magurudumu, nani kweli kwamba malaika hawa wana maumbo ya magurudumu yenye macho mbele na nyuma, kila maahi
Ni viumbe ambao pekee wana macho mengi sana,na hasa kazi yao ni kukibeba kiti cha MUNGU chini ya Makerubi
Daniel 7:9
Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.
Maandiko yanasema unapompokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako MUNGU Baba na mwana hufanya makao ndani yako,maana yake ni kuwa kiti chake cha enzi kinahamia ndani yako.
Sasa nataka upige picha hicho kiti cha enzi ndani yako kikiwa na magurudumu kama hayo ya moto ,kila tatizo lazima litaliwa na huo moto kila ugonjwa,kila uchawi, kama haitoshi juu ya kiti cha enzi kuna malaika wengine wanaitwa makerubi wakilinda hich kiti,maana yake ni kuwa ulinzi utakao kuwa nao sio wa kawaida ni ulinzi wa moto.
Upako wako utakuwa sio wa kawaida kwa kuwa MUNGU mwenyewe ndiye aliyekalia hicho kiti.
Ukiri: Kwa ufahamu huu ninakiri kiti cha enzi na malaika wake ndani yangu katika Jina la YESU


KUNDI LA NNE
VITI VYA ENZI (THRONES)(greek THRONOROS)
Hii pia ni jamii nyingine ya malaika na aina hii ya malaika hukaa mbele za MUNGU kama wazee ishirini na nne
Colosai 1:16
Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Note: Katika biblia ya Kiswahili neno viti limesomeka kama vitu ukiangalia biblia ya kiingereza inasema thrones ambayo maana yake in viti vya enzi.

KUNDI LA TANO
MASERAFI
Hili ni kundi la tano la malaika ambao kazi yao kubwa ni kubeba utukufu wa MUNGU,neno maserafi maanayake ni wanaochoma moto,ni malaika ambao huwaka miali ya moto wakati wote.malaika hawa wana mabawa sita,ambayo kwayo mawili hufunika nyuso zao,mawili huruka na kwa mawili hufunika miguu yao
MUNGU anapotuma malaika hawa kwenye maisha yako huchoma kila kitu ambacho ni kinyume cha MUNGU.
Isaya 6:1-7
MAKUNDI MENGINE YA MALAIKA
CHAYOT (ha kodesh) - malaika watakatifu sana Ezekiel 1 na 10
ERELIM     –Mashujaa- isaya 33:7
HASHMALIM- wenye utukufu, hawani malaika ambao huonekana kama moshi hivi ni malaika ambao hutokea na kupotea Ezekiel 1:4
MALAKIM- Malaika wajumbe
BENE ELOHIM - wana wa Utukufu
ISHIM – Malaika wanaofanana na binadamu
JINSI YA KUTEMBEA NA KUFANYA KAZI NA MALAIKA
1.   TENGENEZA KIU KWAAJILI YAO
Kuwa na kiu na shauku ya kutaka kuwaona, hii itakusaidia kwa kuwa katika ufalme wa MUNGU kiu huvutia udhihirisho wa vitu vya kiroho
Isaya 55:1
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,
Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;
Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,
Bila fedha na bila thamani.


2.   TAMBUA UWEPO WAO NA MCHANGO WAO
Kuna muhubiri mmoja amewahi kusema,”kitu usichokifahamu hauwezi kukisherehekea na kitu usichokisherehekea siku moja kitaondoka katika maisha yako” maneno haya Yana ukweli Sana katika kutembea na malaka
Malaika hutaka ufahamu kuwa wao wapo na usherehekee utendaji kazi wao,si rahisi sana MUNGU kuachilia malaika kwako ikiwa hautambui uwepo wao na umuhimu wao,malaika ni halisi na wapo
Wakati mmoja mtumishi waMUNGU Eubert Angel wa kanisa la Spirit Embassy alikuwa akizungumza na wageni nyumbani kwake lakini gafla wale wagen wakafunguliwa macho na kuona malaika wawili wakiwa wamekaa karibu na sehemu ya kuotea Moto wakizungumza.
Eubert anasema siri kubwa ni kutambua uwepo wao ya kwamba wapo hii itakusaidia wewe macho yako yaweze kufumbuliwa
Mtumishi wa MUNGU Shepherd Bushiri pia Katika moja ya ibada kanisani kwake Malaika walitoke hadharani na kuonekana katika utukufu wao,siri kubwa ni ukiri wa Imani hallelujah.
Ninaamini na ninakiri juu yako kuanzia leo ufahamu wako utajazwa na uwepo wa malaika Paulo anasema
Wakolosai 3:2
Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
Tuyaangali mambo ya mbinguni na kuyatafakari hayo,fahamu zetu zijazwe na mambo ya mbinguni kila wakati,fikiri juu ya malaika,fikiri juu ya mema ambayo MUNGU amekuandalia,mambo ambayo jicho halijawahi kuyaona. Unahitaji kubadilisha mtazamo juu ya vile unayofikiri,
Nimegundua kuwa watu wengi hasa waafrika tuna muda mwingi sana wa kufikiri kuhusu wachawi na majini na mapepo,na hivyo ni vitu pekee ambavyo yunaweza kuvifikiri,na ndio mana vita vyetu haviishi kwa sababu tunashinda tukikiri juu ya mapepo na majini badala ya kukiri mambo ya kiungu





3.   MALAIKA HUMTII MUNGU NA NENO LAKE
Nimeona watu wengi wakikosea sana katika hili,hutaka malaika wawatii wao,utamsikia mtu anasema,naamuru malaika waje kwako,hii ni ajabu sana na si njia ya kibiblia ya kuwafanya malaika wafannye kazi.Kumbuka malaika ni wa MUNGU na sio wa Kwako,ona YESU alivyosema juu ya malaika
Matayo 26:53
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

Neno la msingi nami nitamsihi baba,kwahiyo basi unahitaji kumwomba MUNGU na si kuwaomba malaika,MUNGU ndiye mmiliki wa malaika unahitaji kuomba,
Jambo jengine ni kuwa malaika husikia sauti ya neno la MUNGU na kutii,kwa hiyo unapoomba maombi yako yote huku ukiwa umeambatanisha na neno kuwa na uhakika yakua unawavutia malaika katika kutekeleza neno ulilolitamka.
Maandiko yanasema MUNGU akituma neno lake haliwezi kumrudia bure ni lazima litatimiza kile ambacho limetumwa.
YESUni Neno na neno ni YESU.



4.   KUSUDIA NA KIRI MARA KWA MARA JUU YA UWEPO WAO KWAKO.
Kama tulivyotangulia kuona malaika wanahitaji Imani ya kukiri,kili kwamba wapo hata kama huwaoni ,endelea kukiri kwa imani kwamba wapo,lazima ukiri wako uzae matunda.
Ayubu 22:28
Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako

5.   ISHI KATIKA ROHO
Malaika ni viumbe wa Kiroho wanaishi katika Roho,ni muhimu kuishi katika Roho ili uweze kuwa na muunganiko nao.maandiko yanasema mwili na roho vimepingana tangia mwanzo, maana yake kwa mtu wa Mwilini si rahisi na kutambua mambo ya rohoni
Kwa hiyo basi kuishi katika roho ni ufunguo wa Kwanza wa kutembea na kuishi na malaika
6.   KUWA MKALIMU(hospitality)
Tumeona moja kati ya kundi la malaika linaitwa Ishim,hawa ni malaika wanaofanana na wanadamu na wakati mwengine hutokea katika mwili,maandiko yanasema tuwe wakarimu kwa sababu wengine walipokea malaika pasipo wao kujua,
Ukarimu na upendo huwavutia sana Malaika kuliko unavyoweza kufikiri,kwa ukarimu wa Ibrahimu alipokea malaika na hivyo aliweza kumwokoa ndugu yake Lutu,lakini pia kwa kukosa ukarimu sodoma na gomora viliangamizwa kwa moto kabisa.
Amua leo kuwa mkarimu kwa wageni hasa jamii ya watu wa MUNGU.

Kwa kumaliza ni muhimu sana kufahamu ya Kuwa malaika hufanya kazi na wale watakaourithi wokovu maana yake ni lazima kuokoka kwanza,ni lazima jina lako liwe limeandikwa mbinguni.
Hivo bas ni Muhimu kuokoka na kumfanya YESU kuwa Bwana na Mwokozi wako,YESU ni neno na Neno ni YESU,Ndani yake ndimo kuna uzima ambao ni nuru yako Hapa Duniani na Mbinguni.
Ukiwa tayari kuokoka tafadhali tujulishe kupitia namba hii nasi tutakuhudumia
Maombi ya Moto ya kusababisha malaika kuingilia hatima yako na kukusaidia
-maombi haya yamevuviwa na unapoomba maanisha na nivizur sana kuomba maombi haya ukiwa umefunga au wakati wa usiku wa manane

1.   Fadher in the name of Jesus Christ I repend of my sins,as I enter into prayer relm,cover me with your blood.

Baba katika jina la Yesu ninatubu Dhambi zangu zote,na ninapoingia katika ulimwengu wa maombi ninajifunika kwa Damu yako

2.   Father in the name of Jesus,command angels to intervene in my situation,my situation is urgency and it needs angelic intervertions

Baba katika jina la Yesu Amuru malaika wako waingilie hali yangu,hali yangu ni ya dharula na inahitaji mwingilio wa kimalaika

3.   every  evil spirit persuing my life I invite angel to destroy you in Jesus name,spirit of setback,spirit of poverty,spirit of killing and stealing in the name of Jesus be destroyed

Kila roho chafu inayofuatilia maisha yangu ninaalika malaika waiharibu katika jina la Yesu,roho ya kurudi nyuma,roho ya umasikini,roho ya uuwaji na wizi viharibiwe katika jina la yesu

4.   Kila vioo vya kipepo vinavyo mulika maisha yangu ili kuayaharibu kutana na malaika wa moto katika jina la Yesu
Every evil morror monitoring my life meet the angel of fire in the name of Jesus

5.   Naalika malaika na ninakiri uwepo wa malaika katika kila eneo la maisha yangu katika Jina la Yesu

I invite and confess  the presence of Angels in every area of my life in Jesus Mighy name.

6.   Asante Mungu Baba,asante Yesu Kristo,Asante Roho Mtakatifu


0763712031/0769355558
YESU NI BWANA.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni