COMMENTS


Jumamosi, 4 Juni 2016

SADAKA



AINA ZA SADAKA NA UTOAJI WAKE
tunapoanza kuangalia juu ya sadaka ni muhimu kwanza kabla hatujaangalia kuhusu sadaka  tuangalie mitazamo hasi juu ya sadaka
1.     Sadaka sio msaada
Watu wengi hudhani ya kuwa sadaka ni msaada ambao mtu anatoa katika ualme wa Mungu,au ni msaada kwaajili ya kupeleka injili,au msaada kwaajili ya nyumba ya mchungaji au mtumishi yeyote wa Mungu
Hapana huo ni mtazamo ambao sio wa kimaandiko hebu tuangalie hii
Warumi 11:36
36Kwa maana vitu vyote vyatoka Kwake,
viko Kwake na kwa ajili Yake.
Utukufu ni Wake milele. Amen.
1 cor 8:6
6Lakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vyatoka Kwake na kwa ajili Yake sisi twaishi na kuna Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa Yeye vitu vyote vimekuwepo na kwa Yeye sisi tunaishi
Katika mistari hiyo hapo juu utaona na kugundua kuwa vitu vyote ni mali ya bwana na hakuna kitu kinachotoka kwako au kipo kwa uwezo wako,vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa uweza wake na kwaajili yake,
Kwa hiyo basi ni kosa kufikiri ya kuwa unapotoa sadaka unakuwa unatoa msaada kwa kanisa au ufalme wa mungu au Kwa mtumishi wa Mungu.
2.     SADAKA SIO KILE UNACHOTOA
Sadaka halisi sio kile unachotoa bali kile Kinachokusukuma kutoa,sadaka sio ile fedha unayoweka katiaka kapu la sadaka bali ni ule moyo wako unaokusukuma kutoa
Luka 21:3
Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya hekalu.2Akamwona pia mwanamke mmoja mjane maskini, akiweka humo sarafu mbili za shaba. 3Yesu akasema, “Amin, amin nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo sadaka kubwa zaidi kuliko wengine wote.
Watu wengi huwa wanafanya makosa wakifikiri wingi wa sadaka anayotoa ndiyo inayomfanya mungu kuweza kuachilia Baraka katika maisha yao,bila kukumbuka kuwa ni moyo ambao mungu huangalia
Hebu tuangalie huo mfano hapo juu utaona ya kuwa Yule mwanamke mjane pamoja na kuwa alitoa sarafu moja tuu na wengine wakatoa dhahabu na pesa nyingi,alionekana kuwa mtoaji bora wa siku hiyo. Ni kitu gani kilafanya akaonekana bora kuliko wengine,ni ule moyo wake,Ni ile nguvu au msukumo wa utoaji na kwa sababu hiyo pamoja na kuwa alitoa kiasi kitdogo lakini alionekana ametoa kitu kikubwa zaidi ya wengine.
1falme 17:13
13Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unifanyizie mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyonavyo kisha uniletee na ndipo utayarishe cho chote kwa ajili yako na mwanao. 14Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: “Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.’’
15Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. 16Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno la BWANA alilosema Eliya.
Sasa angalia jambo jingine hapa,na utagundua kuwa huyu mwanamke wa serepta pamoja na mwanamke Yule mjane katika luka 21:3 wanakitu kinachofanana kinachofanya waonekane kuwa bora zaidi ya wengine,ni ile nguvu inayo wasukuma katika utoaji,wanatoa sio kwa sababu wanavyovingi bali ni kwasababu ya moyo wa imani na moyo wa kupenda.
Hivo bas kwa kukazia nataka ufahamu kuwa sadaka sio kile unachotoa ila Kipimo cha nguvu inayosukuma sadaka.
Hebu tuangalie mfano wa Mwisho
Mwanzo 22:1-2 &11
Uthabiti wa Abrahamu
KujuaBaadaye Mungu akamjaribu Abrahamu.Akamwambia, “Abrahamu!’’ Abrahamu
akajibu, “Mimi hapa.’’
2Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojwapo nitakaokuambia.’’
12Akamwambia, “Usimdhuru kijana,
wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.’’
Napenda uone jambo katika huo mfano hapo juu ambayo nimekuonesha,na unaweza ukaona ya kuwa Mtazamo wa Mungu juu ya Ibrahimu haukuwa juu ya sadaka bali ni kutaka kujua uchaji wa ibrahimu na kipimo cha kujua uchaji wake kilikuwa ni kumjaribu ibrahimu kupitia kile ambacho yeye anakipenda zaidi ya kitu kingine
Kumbuka sababu nyuma ya sadaka haikuwa isaka bali ni uchaji yaani Kipimo cha utii na upendo wa ibrahimu kwa Mungu.
Sio watu wengi wanaelewa kilichofichwa ndani ya andiko hilo hapo lakini hebu tuangalie  kidogo kwa ufupi
Mungu alimwahidi ibrahimu ya kuwa angembariki na kumpa uzao,na Mpaka kufikia mwanzo 20 Mungu alikuwa ametimiza ahadi yake kwa ibrahimu maana maandiko yanasema
Mwanzo 24
Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee na mwenye miaka mingi, BWANA alikuwa amembariki katika kila njia.
Biblia ya kiswahli cha kivita inasema Mungu alikuwa amembariki ibrahimu akatika kila kitu
Mpaka wakati huo ahadi ya Mungu ilikuwa tayari imetimia isipokuwa katika uzao,na mwazo 22 mungu akatimiza ahadi yake ya uzao kwa ibrahimu. Sasa Basi Bwana Mungu alitaka kujua ikiwa Moyo wa ibrahimu bado alikuwa tayari kuendelea kutii na kumpenda Mungu pamoja na kuwa Mungu alionesha kumbariki tayari.
Watu wengi mara wanapobarikiwa hupoteza kabisa moy wa Kumpenda Mungu na Kumtafuta,unaweza ukaona wakati mtu akiwa na mahitaji hapo ndipo anapomtafuta Mungu kwa moyo wote na kuonesha upendo mwingi kwa Mungu,lakini mara anapofanikiwa na kupata anachotaka,hupoteza ladha ya Mungu katika maisha yake.
Kwa hiyo basi kutokana na sababu hiyo Mungu aliamua kumjaribu ibrahimu ili kujua kipimo cha upendo wake.




3.     SADAKA SIO TAKRIMA/RUSHWA.
Katika huduma yangu nimeona kuna makosa makubwa sana ambayo hufanyika katika mwili wa Kristo,unaweza ukaona watumishi wa Mungu wanashawishika kuwapa nafasi watu Mbalimbali kwa sababu tu sadaka yao kanisani huwa ni kubwa na ya kwamba wanaouwezo kidogo kifedha,hili ni kosa kubwa
1samwel 16:7
7Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa.BWANA hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini BWANA hutazama moyoni
Mungu hatazami vile mtu alivyo kisura au kifedha katika hali yoyote bali hutazama moyo wa Mtu,yeye haangalii kiasi cha sadaka mtu anachopeleka bali hutazama moyo wa upendo na Uchaji
Hivo basi sisi kama watumishi wa Mungu tusiwe wepesi kupendelea watu kwa sababu ya Muonekano wao wa Nje(Material things). Sisemi kuwa ni vibaya ama haifai kuchagua Mtu mwenye uwezo,hapana bali ni muhimu Mwomba Mungu kwanza kabla ya Kuchagua
Luka 6:12
12Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.13Kulipopambazuka akawaita wanafunzi Wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume: 14Simoni aliyemwita Petro, Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, 15Mathayo, Thomasi. Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote, 16Yuda mwana wa Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye ndiye aliyemsaliti Yesu.
Uchaguzi wetu juu ya nani awe msaidizi katika huduma unahitaji sana kufata hiyo kanuni ambayo yesu alianza nayo
Chochote kinachochaguliwa kwa mwili hufanya vitu vya mwilini na wala si vitu vya kiroho
Isaya 11:2
3naye atafurahia kumcha BWANA.
Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa
macho yake,
wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa
masikio yake,
hivo basi hata mtoaji asitoe sadaka akitegemea kupata kitu toka kwa Mtumishi au Mchungaji bali atoe akitegemea kupata kitu kutoka kwa Bwana.
Sasa basi baada ya kuangalia maana mbalimbali hasi(negative) kuhusu sadaka tuangalie sasa nini Maana ya sadaka.



SADAKA NI NINI
1.     Sadaka ni Nguvu ya upendo/mtazamo wako Kwa Mungu inayodhihirishwa kupitia vitu au Kitu
Kama tulivyoona katika vipengere vilivyopita ya kuwa sadaka ni ile nguvu nyuma ya sadaka,au kwa lugha nyepesi ni lile lengo linalokupelekea kutoa sadaka,mara nyingi matokeo ya kile kinachotolewa hutokana na moyo wa mtu ulivyo.
Shida ya sadaka ya kaini haikuwa katika kile alichokitoa bali ule Moyo wake a ndani/lengo na mtazamo wake juu ya Mungu
Tunasoma
Mwanzo 4:4
katika baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. BWANA akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, 5lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.
6Kisha BWANA akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 7Ukifanya lililo sawa, hutakubalika?Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.
Unaweza ukaona nguvu iliyokuwa nyuma ya sadaka ya abeli ndiyo iliyomfanya abeli aweze kutoa kilichobora, lakini pia unaweza ukaona kaini naye kutokana na moyo wake kutokujali,na kutokumpenda Mungu alijikuta akimkasirikia Mungu kwa Kuwa sadaka yake haikukubaliwa.
Tunachokiona hapa ni kuwa Mungu hakuangalia sadaka bali aliangalia Moyo wa sadaka /lengo la sadaka au msukumo uliopo wa utoaji ulilenga kitu gani.
Sasa basi tumesema sadaka ni nguvu ya Upendo au mtazamo ulionao juu ya Mungu.

Waebrania 10:10
10Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.
Yohana 3:16
16‘‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kwa Yeye ulimwengu upate kuokolewa
Ukiangalia hiyo mistari hapo juu utaona kuwa imebeba maana halisi ya sadaka katika vipengele vyake
Sababu ya Mungu kumtoa Yesu kama sadaka ni kwa sababu aliupenda ulimwengu,ni upendo ndio uliomsukuma mungu kumtoa yesu kuwa Sadaka.
Katika hili tunaweza kujifunza kuwa kipimo cha upendo wako kwa Kungu ndicho kinachoamua ni kiasi gani cha sadaka unahitaji Kutoa,au thamani ya sadaka yako inatokana na kipimo cha upendo wako
Maandiko yanasema Mungu alimtoa Mwanae wa Pekee,maana yake ni kuwa alitoa kile alichonacho.
Mungu alikuwa na Mtoto mmoja tu,hakuwa na watoto wengi,ni mmoja tu na wapekee,huyo ndiye aliyekuwa kila kitu kwake, kwa lugha ya sasa tunaweza kusema yeye ndiye aliyekuwa Jicho na roho ya mungu.yesu alikuwa kila kitu Kwa Mungu baba
Isaya 53:2
2Alikua mbele yake kama mche mwororo
na kama mzizi katika nchi kavu.
Yohana 1:14
14Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,
amejaa neema na kweli.
Yesu hakuwa mmoja wa watoto wa Mungu,alikuwa mwana Pekee wa Mungu. Uzao pekee wa Mungu.
Lakini kutokana na upendo wa Baba kwetu akaamua kumtoa yesu kristo kwajili yetu.
Ni upendo juu ya Ulimwengu ndio ulimsukuma Mungu kumwachilia Yesu.
Yohana 15:13
13Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
angalia tena sababu ya yesu kuutoa uhai wake kama sadaka ilikuwa ni upendo wake kwetu na Kwa baba Yake.
Hivo basi ni muhimu kuliweka hili moyoni ya Kuwa sadaka sio kile unachotoa bali ni ile nguvu ya upendo wako kwa Mungu,na kazi yake,na watumishi wake ndio inayokusukuma kutoa
Usitoe kwa sababu unahitaji kusaidia na ndani yako hauna msukumo wowote,utakuwa unapoteza sadaka yako.
Kabla ya kutoa ni muhimu kwanza kufikiria juu ya yale ambayo Mungu ameyafanya katika maisha yako,fikiri juu ya upendo wake,rehema zake,fikiri juu ya utukufu wake kwako,ulinzi wake,pumzi yake na vile Mungu alivyokubariki,hakafu una unadeni kiasi gani katika kumpenda yeye kama yeye anavyokupenda,ona deni la kupenda kazi yake kama yeye anavyopenda kazi zako,kwa njia hiyo utajikuta unazaisha chemichemi ya upendo baina yako na Mungu.
Upendo wako usisukumwe na kitu chochote isipokuwa upendo wa Mungu kwako.
Mungu haitaji kitu kingine kwako ila haya
Hosea 6:6
6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,
kumkubali Mungu zaidi kuliko sadaka za
kuteketezwa.
Maana yake ni kuwa Mungu hahitaji mamilioni au mia tano yako,bali ule moyo wa upendo ndio ukusukume kutoa hicho unachotoa,kwa kuwa kile unachotoa ndicho kitakachodhihirisha kiasi cha upendo wako kwake.
Ombi: Baba ninaomba unipe neema ya Kukupenda wewe na kujitoa kwaajili yako na Kazi yako na watumishi wako katika Jina la Yesu.











AINA ZA SADAKA
1.                 SADAKA YA MALIMBUKO
Kutoka 13:12
12inakupasa kumtolea BWANA mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya BWANA. 13Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo, lakini kama hukumkomboa, utamvunja shingo yake. Kila mzaliwa wa kwanza mwanaume miongoni mwa wana wenu utamkomboa.
Sadaka ya malimbuko ni sadaka inayohusika zaidi na wazaliwa wa kwanza,ni sadaka ya ukombozi inayotakasa kila mzaliwa wa Kwanza,na Kumkabidhi kwa Bwana.
Limbuko maana yake ni mzaliwa wa Kwanza,na mzaliwa huyu wa kwanza anaweza akawa wa wanyama au,binadamu au ndege.
Na maandiko yanasema utamtolea bwana kila mzaliwa wa Kwanza kama sadaka lengo likiwa kutakasa ama kubariki wazaliwa wengine
1korintho 15:20
Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu,limbuko lao waliolala,kwa maana kwa kuwa mauti ililetwa na Mtu kadhalika  na kiyama ya wafu ililetwa na mtu,kwa kuwa kama katika adamu wote wamekufa,kadhalika na katika kristo wote watahuishwa.
Sasa basi katika mistari hiyo hapo juu kuna kitu nataka tujifunze.
Yesu Kristo ni limbuko/au mzaliwa wa kwanza katika hao walio kufa,maana yake yeye ni mzaliwa wa kwanza kuwa hai kati ya wale waliokwisha kufa na hivo basi kwa sababu yeye ni mzaliwa wa kwanza katika waliokufa anao uwezo wa kuwafufua wengine ambao wamelala mauti
Kwa tafsiri nzuri ni kuwa Kwa sababu yesu ametolewa sadaka kama limbuko sadaka yake inaouwezo wa kuwahuisha hata wale ambao walikuwa wamekufa.
Lengo la Mungu kuleta sadaka ya malimbuko ni kusababisha mpenyo wa Baraka za Mungu katika vizazi vinavyofuata,kama ni vya wanyama au vya mimea au ni watu.
Tunapo mtazama mzaliwa wa kwanza kama lango la vizazi katika familia ni muhimu tukajua ya kuwa ili kuruhusu Mungu kuingilia mtililiko wa vizazi vyako na kufanya kile alichokiahidi katika isaya 54:13
13Watoto wako wote watafundishwa na BWANA,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu
unahitaji kumwachilia mtoto wako wa Kwanza kama sadaka ya limbuko.
Kimsingi inatakiwa kila mzaliwa wa Kwanza anapozaliwa apelekwe madhabahuni na aachwe pale kwa sababu huyo sio wa Kwako bali ni wa Bwana Mungu
Kutoka 34:19
19“Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ng’ombe au wa kondoo au mbuzi. 20Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume.
“Mtu ye yote asije mbele zangu mikono mitupu.
lakini kwa sababu za kiungu,Mungu ameamuru kumkomboa maana yake ni kutoa fedha kama sadaka badala ya Mtoto kulingana na thamani utayoona kwa Mtoto wako na kulingana na uwezo ulio nao.
Luka 2:23
23(kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana”), 24pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa, katika Sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa
Unaweza ukaona ya kuwa Hata yesu Kristo alihitaji kufanya hivo kwaajili ya vizazi vinavyofuata vya mariamu na Yosefu.
2.                 SADAKA YA MBEGU
Mwanzo 1:29
29Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa kwa ajili ya chakula chenu,
Sadaka ya mbegu ndio sadaka inayotawala Kanuni ya kupanda na Kuvuna
Tunasoma katika
Mwanzo 8:22
22“Kwa muda dunia idumupo,
wakati wa kupanda na wa kuvuna,
wakati wa baridi na wa joto,
wakati wa kiangazi na wa masika,
mchana na usiku kamwe havitakoma.’’
Ni amri ya Mungu ya Kuwa Kdili nchi Idumupo majira haya ya Kupanda na kuvuna hayata badilika,na hivyo basi kuwa ni kanuni ya uzazi kutoka kizazi hadi kizazi
Tunapoongelea juu ya sadaka ya Mbegu tunazungumza juu ya sadaka ambayo ina lengo la kusababisha vitu katika maisha yako inapoachiliwa katika udongo mzuri(madhabahu)
Sadaka hii huleta matokeo sawa na Mbegu za kawaida na hutii kanuni ya Mavuno inayosema “chochote Mtu apandacho ndicho atakachovuna”
Galatia 6:7
7Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi.Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Kulingana na kanuni ya uumbaji Mungu ameumba kila kitu kuwa na mbegu ndani yake,na mbegu hiyo inapopandwa kutoa matokeo yanayofanana na kitu kilichokizaa.
Kadhalika unapoachilia sadaka hii tegemea ya Kuwa kile kile ulichopanda ndicho utakachovuna.
Sasa basi hebu tuangalie Tabia za Mbegu ili pia tuweze kuelewa matokeo tutakayopata mara tunapopanda sadaka hii madhabahuni.


A.     Mbegu inapopandwa hufa kwanza ili kuchipua tena
Yohana 12:24
24Amin, amin, nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.
Ili mbegu iweze kuota ni lazima iachiliwe halafu ife,lakini isipoachiliwa basi hubakia kama kama mbegu na isilete Matunda yoyote,natamani uelewe kuwa mbegu inahitaji Kufa ili iweze kuishi,haiitaji kunyauka inahitaji kufa
sasa basi kama unahitaji sadaka yako kujizalisha mara mia huna budi kuiachilia katika madhabahu sahihi ya Mungu(udongo Mzuri) ili iweze kuinuka tena
tunapo angalia mfano wa mpanzi tunajifunza kuwa si kila mahali unapoachilia mbegu yako basi kuna weza kukuletea matunda,Kupitia mfano huu Tuangalia madhabahu nne ambayo  mbegu inaachiliwa na matokeo yake
4Alipokuwa akipanda, baadhi zikaanguka kando ya njia, ndege wakaja na kuzila. 5Nyingine zikaanguka sehemu yenye mawe, ambapo hapana udongo mwingi. Zikaota haraka kwa sababu udongo ulikuwa hauna kina. 6Lakini jua lilipozidi, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikuwa na kina. 7Mbegu nyingine zilianguka katikati ya miiba, miiba hiyo ikakua ikazisonga.8Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri ambapo zilitoa mazao, nyingine mara mia moja, nyingine mara sitini na nyingine mara thelathini.

1.     madhabahu iliyo karibu na njia
madhabahu hii ni madhabahu ambayo hijakaa sawa na Mungu,hakuna udongo(Uwepo wa Mungu) ni madhabahu ambayo mara tu unapopanda mbegu yako adui huja na kuichukua,maana yake mbegu yako hutumiwa kwaajili ya mambo yasiyo ya Ufalme wa Mungu.
Kumbuka madhabahu imo ndani ya Moyo wa Mtumishi wa Mungu,na sio ndani ya kanisa. Na ndo mana unapotoa sadaka sadaka haziishii kukaa ndani ya makapu pale mbele kwenye miambari.
Wakati wa kwanza(agano la kale) Mungu aliruhusu madhabahu za kimwili kujengwa kwa Mawe ,kuni na mote mahali alipopachagua yeye Mwenyewe,na sadaka yako ingeweza kutolewa hapo. Ni kwa sababu agano lile lilikuwa ni kivuli cha agano jipya
Katika kipindi hiki Mungu hujenga madhabahu ndani ya Mtumishi kupitia Neno(mawe),Maombi(kuni) na Moto(roho Mtakatifu).
Hivyo basi unapotoa sadaka yako,ile sadaka inatakiwa kuliwa na Mtumishi wa Mungu na inapoingia ndani yake iingie katika madhabahu ambayo Mungu mwenyewe ameijenga.
Sasa basi kama madhabahu hii imejengwa njiani yaani haikujengwa na roho mtakatifu bali imejengwa kwa tama na upako basi hata ukipanda haita ota wala haita bakia.
2.     Madhabahu iliyojengwa kwenye Mwamba
Mwamba uliozungumzwa hapa ni mwamba kama jiwe, mahali pagumu mahali ambapo hapana udongo wa Kina, katika eneo hili Mbegu huweza kufa lakini haiwezi kuota kwa sababu udongo wake hauna kina
Maana yake ni kuwa madhabahu hiyo inawezekana ikawa imejengwa na Mungu lakini kwa sababu Haina nguvu ya mungu ya Kutosha basi mbegu hufa na hivyo haioti kabisa.


3.     Madhabahu iliyokwenye miba
Aina hii ya madhabahu ni madhabahu ambayo kimsingi inakuwa imejengwa na Mungu mwenyewe na ipo katika udongo mzuri, lakini kwasababu ya kusongwa songwana mambo ya Dunia kila mbegu inayopandwa hapa huota lakini hitoi matunda.
Unapopanda sadaka yako ya aina hii Tegemea kupata kiasi kile kile ulicho panda na si zaidi.Mtu aliyebeba madhabahu hii ni mtu mwenye wito wa kimungu Ndani yake lakini shida yake kubwa ni kuwa hajatulia na Mungu vizuri.
4.     Madhabahu iliyo katika Udongo Mzuri
Hii ni madhabahu ambayo iko vizuri na Moto wake unawake,ni madhababu inayotembea na uwepo wa Mungu, nanapopanda Mbegu yako katika Madhabu hii tegemea kuvuna mia mara thelasini mara sitini(100x60x30=???)
B.      Mbegu huzaa kile ambacho kinafanana na ilipotoka
Mwanzo 1:29
29Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa kwa ajili ya chakula chenu,
Hii ni muhimu sana Kufahamu,ya Kuwa kila Mbegu huzaa kulingana na aina yake,kwa hiyo ninamaana ya kuwa Unapopanda upendo tegemea kuvuna Upendo
Watuweng hutamani sana Kupendwa lakini wao wenyewe hawako tayari kujitoa kupenda.
Kumbuka kila kitu kinachokuzunguka ni Mbegu,na kila tendo unalolifanya ni Mbegu,huzaa mara nyingi unapopanda.
Maandiko yanasema

Luka 6:38
38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.”
Unapoamua kutoa,katika mfumo wa Mbegu jua kuwa kile kile unachotoa ndicho utakachopokea mara dufu na kushindiliwa kabisa
Kama ukipanda mabaya maana yake utavuna mabaya
Mithali 17:13
13Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema,
kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba
yake.
Vile Mungu amekuumba,ameyafanya maisha yako kuwa katika mfumo wa Mbegu,na kwa hiyo chochote unachopanda tegemea ndicho utakachovuna.
C.      Mbegu huamua kiasi cha Mavuno
Tabia nyengine ya Mbegu ni kuwa huamua kiasi cha mavuno kutokana na kiasi ulichokipanda.
Hauwezi kupanda mbegu moja ya mahindi halafu utegemee kuvuna shamba zima au gunia la mahindi hiyo haiwezekani.
D.     Mbegu Hupandwa kulingana na Msimu
Unahitaji kujua majira ya kupanda Mbegu yako na si kila wakati unapoona unataka kupanda ni majira.
Ninakushauri upande mbegu yako wakati ambapo kuna uhitaji udongo inahitaji mbegu.
Lakini pia unaposikia neno la kinabii likiachiliwa juu ya maisha yako, huo ndio wakati mzuri sana Kupanda.
KUJIFUNZA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA MBEGU YAKO KUZAA KUPITIA NENO LA KINABII.

Mwanzo 27:1-8
Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa akamwambia, “Mwanangu.’’
Akajibu, “Mimi hapa.’’
2Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu. 3Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu. 4Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.’’
5Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta, 6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, 7‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za BWANA kabla sijafa.’ 8Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: 9Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyotaka. 10Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.”
Kila mtumishi wa Mungu ananeno la kinabii kwaajili ya watu wa aina Fulani na neno hili linapoachiliwa huleta matokeo yasiyo yakawaida katika maisha yako.
Lakini ni muhimu kujua jinsi ya kufanya neno hili likaachiliwa juu yako kwaajili ya kuleta mabadiliko
Lakini pia napenda ufahamu kuwa neno hili haliachiliwi mpaka umepanda mbegu au umetoa sadaka
Katika mistari hiyo hapo juu unaweza ukaona wakati ambapo isaka anakaribia kufa alijua ya kuwa anahitaji kuachilia muendelezo wa Baraka juu ya watoto wake,lakini pia alifahamu ya kuwa sio rahisi kwa neno hili kutoka likiwa na uwezo wote wa kuleta mabadiliko mpaka pale ambapo kitu kitafanyika.
“Chazah” hili ni neno linalo maanisha mwamko wa ndani wa nabii au mtumishi wa Mungu unaosababisha kuachiliwa kwa Baraka yako.mwamko huu huachiliwa pale Mtumishi anapofurahi ndani yake,ni upako maalumu ambao huachiliwa tu pale Mtumishi wa Mungu anapofurahi kutokana na jambo ambalo umelifanya
Hebu kwa haraka tuangalie baadhi ya mifano ya kibiblia.
1sam 9:7
7Sauli akamwambia mtumishi wake, “Kama tukienda, tutampa nini huyo mtu? Chakula kimekwisha kwenye mifuko yetu. Hatuna zawadi ya kumpelekea huyo mtu wa Mungu. Je tuna nini?’’
8Mtumishi akamjibu tena, akasema, “Tazama, nina fedha robo shekelia. Hiyo nitampa huyo mtu wa Mungu ili aweze kutuambia tuende kwa njia ipi.’’ 9(Zamani katika Israeli, kama mtu alikwenda kuuliza neno kwa Mungu, angalisema, “Njoo na twende kwa mwonaji,’’ kwa sababu nabii wa sasa alikuwa akiitwa mwonaji
Unaweza ukaona jamii ya Israel walijifunza juu ya jambo hili ambalo ninakufundisha leo,kufanya kitu kwaajili ya Mtu wa Mungu ili Neno la kinabii liweze kuachiliwa kwaajili yako
Si watu wengi sana huwa wanaelewa hii kanuni na nimeona wengi huona kama ni wajibu wa mtu wa Mungu kufanya kitu kwajili yao bila wao kufanya kitu kwaajili yao,hii ndio mana wengi wanakuwa kanisani na nimasikini na hali Mtu wa Mungu analoneno kwaajili yao ambalo linaachiliwa kwa njia ya kupanda Mbegu.
Huwezi ukakwepa jambo hili kama unahitaji kuingia katika ulimwengu wa mafanikio ya kiungu,ni lazima Ufanye hivo.
Jufunze kugusa Moyo wa mtumishi wa Mungu kwa kua ndio Madhabahu ya Mungu ilipo.
1falme 17:13
13Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unifanyizie mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyonavyo kisha uniletee na ndipo utayarishe cho chote kwa ajili yako na mwanao. 14Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: “Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile BWANA atakapoleta mvua juu ya nchi.’’
15Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. 16Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno la BWANA alilosema Eliya.
Angalia mfano mwengine hapo juu,unaweza jiuliza kwa nini Eliya alisema afanyiwe yeye mkate ? hii ni kwa sababu hakuna nabii anayeweza kuachilia Baraka ikiwa ana njaa au nyumbani kwake kuna njaa,hivo ili kuachilia Nguvu ya baraka alihitaji kushiba kwanza yeye na moyo wake ufurahi ndio aweze kuachilia.
Na unaweza ukaona baada ya kufanya hivyo nini kilitokea.
Kuna mifano mingi sana ambayo tukianza kuielezea tutamaliza siku nzima.
Kwa kumalizia sadaka aina Mbegu ni sadaka kwaajili ya Kuongeza hema yako na Mipaka yako .Isaya 54



3.                  FUNGU LA KUMI
sadaka ya Fungu la kumi ni kanuni ya ufalme wa Mungu,na imefungwa pia katika mfumo wa kikanuni. Yaani hii ni sehemu ya Kumi ya Mapato yako yote unayoyapata.
Mwanzo 14:20
20Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,
ambaye amewaweka adui zako mkononi
mwako.’’
Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.
fungu la kumi ni sadaka ambayo haikuanza leo au jana ni sadaka ambayo imekuwepo hata kabla ya kuwepo kwa sheria,Hii ni Kanuni inayofungua malango ya Balaka katika ghala za Ufalme wa Mungu.
Kwa lugha nyepesi na ya Kisasa ni Kuwa fungu la Kumi na kama kodi ya ufalme inayokufungulia njia ya kupokea vitu kutoka katika ufalme wa Mungu kama raia wa ufalme
Fungu la Kumi ni kanuni ambayo Mungu ameiweka ili kusukuma maisha ya watumishi wa Mungu ili naye Mungu aweze kukufungulia Milango ya Baraka.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya maisha yako na ya Mtumishi wa Mungu,na kwa kadri mtumishi wa Mungu anapofanikiwa ndivyo na wewe unavyopata nafasi ya kusitawi,hii ni njia ya Kibiblia
Zaburi 133
Tazama jinsi ilivyo vema na
kupendeza
wakati ndugu wanapoishi pamoja
katika umoja!
2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa
kichwani,
yakitiririka kwenye ndevu,
yakitiririka kwenye ndevu za Aroni,
mpaka kwenye upindo wa mavazi yake.
3Ni kama vile umande wa Hermoni
unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni.
Kwa maana huko ndiko BWANA
alikoamuru baraka yake,
naam, hata uzima milele.
Hilo andiko unaloliona linafundisha kanuni za mtiririko wa Upako wa Kufanikiwa(mafuta),maandiko yanasema mungu anapoachia mafuta,huachia kuanzia katika ndevu za Aron(haruni) na hushuka mpaka kwenye ndevu na mwisho ni kwenye pindo la vazi lake
Vile ulivyo nimatokeo ya Upako unaotoka katika maisha ya mchungaji wako/kiongozi wako wa Kiroho,anapofanikiwa unafanikiwa
Upako huanzia kwa mchungaji(haruni)na hushuka mpaka mwisho wa pindo la vazi lake(kanisa),hauanzii mwisho wa upindo bali juu.
Hivo basi ungu la Kumi ni mlengo wa kuachilia mafuta ya mafanikio kutoka kwa mtumishi wa Mungu yatakayoshuka mpaka chini kabisa ya Mshirika wa Mwisho kanisani.


KWA NINI MUNGU ANATAKA TUTOE FUNGU LA KUMI KWA KANISA.
Malaki 3:10
10Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la. 11Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 12‘‘Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.
Sababu kuu ya kuleta zaka kamili ni ili kiwemo chakula katika nyumba ya Bwana kwaajili ya Makuhani wanaohudumu katika nyumba ya Bwana
Makuhani ni watumishi ambao Mungu amewatenga kwaajili ya utumishi wake.ni kama walawi katika agano la kale,Mungu ameamuru wale madhabahuni,yaani wale sadaka zinazotolewa madhabahuni
1korinth 9:13
13Je, hamjui kwamba, watu wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni, nao wale wahudumiao madhabahuni hushiriki kile kitolewacho madhabahuni?14Vivyo hivyo, Bwana ameagiza kwamba wale wanaohubiri injili wapate mahitaji yao kutokana na injili.
Fungu la kumi na haki yao itokayo kwa MUNGU
Unapoacha kutoa fungu la kumi lililokamilifu maandiko yanasea unamwibia Mungu na hivo kutembea chini ya Laana
Malaki 3:8
8‘‘Je, mwanadamu atamwibia Mungu?Hata hivyo mnaniibia.
‘‘Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’
‘‘Mnaniibia zaka na dhabihu.9Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

Kuna madhara makubwa ya kuto kutoa fungu la Kumi,madhara haya ni pamoja na kutembea chini ya Laana,na unaporuhusu laana juu yako maana yake ni kuwa hautakuwa na maendeleo yoyote yale.
Fungu la kumi linatakiwa kutolewa na Mtu mmoja mmoja, Kanisa,na Nchi,ili mungu aweze kuleta ulinzi na Baraka katika maisha yetu.
Malaki 3:10
10Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘‘nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la. 11Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 12‘‘Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.











4.                  SADAKA YA SHUKRANI
Kumbukumbu:8:18
Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
sadaka ya kushukuru ni sadaka Muhimu sana kwaajili ya muendelezo wa Agano la Baraka,Ni sadaka inayoongozwa na msukumo wa Moyo wa Shukrani,na unyenyekevu mbele za Bwana
sadaka hii ipo kutangaza matendo ya Mungu aliyoyafanya katika maisha ya mtu,ni kumbukumbu ya kile alichokifanya Mungu katika maisha yako,
biblia inasema





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni