UKOMBOZI WA MILKI YAKO NA JINSI YA
KUPANUA MIPAKA YAKO KWA NJIA YA KUOMBA.
Angalizo
Tafadhali unaposoma kitini hiki jitahidi sana
kufuata na kuomba kila ombi ambalo nimeliainisha ili kupata matokeo yaliyo bora
zaidi
Usipige kopy kitini hiki ni vizuri ukakinunua
kutoka kwa mwandishi kwa gharama yake ili Mungu akubariki.
UKOMBOZI WA MILKI YAKO NA JINSI YA
KUPANUA MIPAKA YAKO KWA NJIA YA KUOMBA.
Isaya 54:1-3
Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga
kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko
watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA. 2Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako;
usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. 3Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako
watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
Tunajua ya kuwa Mungu ametufanya kuwa wafalme na makuhani na
ametupa kusudi la kumiliki katika nchi, kumiliki kwetu na kupanuka kwetu
hakutatoke tu bila kujifunza ni jinsi gani tunaweza kufanya kutokea
Unaweza ukaona ya kuwa kazi ya kupanua hema na mipaka si kazi
ya Mungu bali ni kazi yako mwenyewe na usipochukua hatua kamwe huwezi
kufanikiwa
Kuna mambo mengine mungu anasubiri uchukue hatua ili kusudi
nay eye apige hatua katika kukusaidia na hi ndiyo sababu ninakuletea muktasari
wa somo hili ili yamkini upate ufahamu na uaze kushughulika
Watu wengi wanajua sana andiko hili ufunuo 5:10
Lakini si wote wamefika katika utukufu wa Andiko hili kwa
sababu hawajui ni nini kinahitajika ili kufika mahali pa juu.
Kwa kuangalia andiko hilo hapo juu la isaya 54 utaona ya kuwa
si Mungu anayekupanulia mipaka bali ni wewe unaye hitajika kupanua mipaka yako,kuna
nafasi kubwa bado ya kumiliki kwako na kuna nafasi kubwa kwajili ya kuzaa vitu
vya Kiroho.
Mtu anakuwa tasa Kwa sababu ya kuto kuchukua hatua ya imani
katika kupanua hema yake na mipaka yake ili mungu aweze kumjaza vitu
Mfano
Kama Yule mwanamke wakati wa elisha asingelichukua hatua ya kwenda kuazima
vyombo kwa majilani zake maana yake vile alivyonavyo vingekuwa ukomo wa ujazo
wake wa kimahitaji
1falme
4
.
Vipi kama petro asingalichukua hatua ya kwenda kumfuata
yesu,maana yake angeendeea kuwa mvuvi wa samaki wakati kuna mahali pa juu zaidi
ya kwenye biashara ya samaki
Vile ulivyo ni matokeo ya mipaka uliyoiweka mwenyewe,unaweza
kwenda mbali na hapo ulipo.
INAANZA NA WEWE KUCHUKUA HATUA
Ni vema kujua Mungu hufanya kazi na watu wa imani
Waebrania 10:38
Hivo usipochukua hatua hawezi kukusaidia,kiasi kile kile
unachopanua ndicho kitakachoamua ujazo wako wa Baraka.
Mungu hutumia kipimo kinachoitwa Kadri ili kuleta Ujazo wa
vitu maishani mwetu,
Efeso 3:20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya
ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo
kazi ndani yetu; 21naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya
milele na milele. Amina.
Angalia mstari niliouchora kwa mstari,hii ina maana ya kuwa unahitaji
kuchukua hatua ya kuongeza nguvu ndani yako ili kumfanya Mungu atengeneze mambo
makubwa katika maisha yako,haiwezekani tu ukakaa ukitegemea Mungu kufaya kitu
kwajili yako kabla wewe hujaanza kwanza
Kumbuka Mungu hutumia kipimo kinaitwa Kadili
Luka
6:27-38
37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi
hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. 38Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na
kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa
kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
neno kwa kuwa ni sawa na neno kwa kadili,kwa hiyo ujazo wako wa Umiliki
na ujazo wa mipaka yako unategemea sana ni kiasi gani umeipanua hema yako na ni
kiasi gani umepanua mipaka yako
mfano kwa mfanya biashara kupata faida kubwa inategemeana na ukubwa wa
Biashara yake,lakini Mtu anaye fanya biashara yake Kukua sio mtu mwengine ni
wewe mwenyewe kwa kuwekeza bila kuchoka.
Mtuwa Mungu ni Muhimu sana kufahamu kuwa katika ufalme wa Mungu vitu
vingi sana huanza na wewe mwenyewe. Mtu mmoja amewahi kuniuliza swali hili,”kwa
nini siku hizi simuoni Mungu katika Maisha yangu nina tatizo gani” Kwa mtazamo
wake alijua kwa Kuwa mimi ni Nabii basi ningeweza kumwambia kuwa unajua laana
za ukoo,au mapepo n.k
Lakini akashangaa ninamfungulia andiko hili
Isaya
55:6-7
6 Mtafuteni
BWANA, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 Mtu
mbaya na aache njia yake,
Na mtu asiye haki aache mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa Mungu wetu,
Naye atamsamehe kabisa.
unaona sasa inaanza na
wewe kumtafuta Mungu,mtafute kwa kuwa yeye anapatikana,halafu Muite maadamu yu karibu inaanza na wewe.
mathayo 7:7-8
7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona;
bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8kwa maana kila
aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Isaya 60:1-3
Ondoka,
uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Usipoomba huwezi
kupata,usipotafuta huwezi kuona.usipondoka huwezi kuangaza.
Ninarudia tena Mungu hutaka wewe uanze Kwanza kisha yeye
atafuata, shidani kuwa watu wengi husubiri Mungu aanze kwanza bila wao kufanya
chochote
Unapoanza kwanza unaithibitisha imani yako kwa Mungu,ndio
maana wengi hawafanikiwi na muda unakwenda bila kuanza kwanza.
Hata unapohitaji Baraka Mungu hutaka uanze kwanza.
Kutoka 23:25
25Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye
atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. 26Hapatakuwa na
mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku
zako nitaitimiza. 27Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako,
nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako
wote wakuonyeshe maungo yao. 28Nami
nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke
mbele yako
Hakuna Dawa nyingine
ya kufanikiwa kiMungu isipokuwa umeanza kwa utumishi.
Sasa basi
umeona kuwa kila kitu kinahitaji uanze ndipo Mungu afanye,sasa ili kufika
unahitaji kupanua hema yako na unahitaji kupanua mipaka yako ili umiliki na
kuwa na ujazo wa Baraka zako
Baraka hazina
Kikomo.
UNAHITAJI KUWA
NA ELIMU YA UKOMBOZI
Si watu wengi
wanaelewa hili suala ya kuwa kila kitu kinahitaji ukombozi ili uweze
kukimiliki,hii ni kwasababu Dhambi ilimpa shetani ulimwengu huu na kuwa milki
yake nan do mana maandiko yanamwita mungu wa dunia hii
Luka 4:5
Akampandisha
juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6Ibilisi
akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi
mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7Basi, wewe
ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.
Dhambi ilimpa
shetani umiliki wa Dunia hii na hivyo unapookoka maeneo yako hayaokoki mpaka
umeyakomboa,nchi yako haiokoki mpaka umeikomboa
Mtu mmoja
aliniuliza swali hili “kwa nini watu wa
Mataifa wanafanikiwa sana kuliko wana wa Mungu,jibu ni rahisi sana
Luka 4:6
6Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari
yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7Basi, wewe
ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako
Shetani humpa
yeyote anayemsujudia kama anavyopenda mwenyewe kwa kuwa vitu vyote ni milki
yake mpaka umevikomboa
Ukombozi ni
njia ya kumpokonya shetani uhalali wa Umiliki. Na shetani akijua hili
amewafunga wakristo wengi sana katika umasikini kwa kuwa hawaelewi umuhimu wa
maombi ya ukombozi,wanadhani ukishaokoka basi ndo umeshapata kila kitu,hapana
hiyo sio njia ya kibiblia.
Hii ndio maana
efeso 6:10
Hatimaye,
mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.11Vaeni silaha
zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.12Kwa maana
kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho.
Maombi ya ukombozi ni
maombi ya nguvu ni maombi ya kukomboa milki,Ardhi mipaka na kila kilicho
chako,vitu vingi viko mikononi mwa adui,tunahitaji kuvikomboa.
NAMNA GANI SHETANI ALIPATA HAKI YA KIAGANO YA
UMILIKI WA VITU VYETU NA MIPAKA YETU.
Kwanza kabisa nataka
ufahamu kuwa vitu vyote unavyoviona havikuwekwa chini ya shetani bali chini ya
Mwanadamu
Mungu alimpa mwanadamu
kuwa mmiliki halali wa kila kitu katika ulimwengu huu
Mwanzo 1:26
Mungu akasema,
Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi. 27Mungu akaumba
mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba. 28Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 29Mungu akasema,
Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na
kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;na
chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu
kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula
chenu; ikawa hivyo.Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema
sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Mungu hakuumba vitu kwaajili ya Shetani bali aliumba kwaajili ya
mwanadamu,ili avimiliki na kuvitawala. Kwa hiyo kuwepo mikononi mwa shetani ni
makosa makubwa sana ambayo yanahitaji sana yarekebishwe.
Mwanzo 1:26
Mungu alihitaji kutengeneza Aina yake itakayo ishi katika uliwengu wa
nyama na Damu,na kama Mungu alivyo mfalme wa yote ndivyo mwanadamu atawale na
awe mfalme wa vyote katika ulimwengu wa Damu na Nyama.
Na hii aina yake ni mwanadamu. Sasa basi unapoona umiliki wako umekuwa
ni umiliki wa Mwingine ambaye hakuwa na haki hapo kwanza,inamuhuzunisha Mungu.
DHAMBI
Kupitia Dhambi shetani alipata nafasi ya kutawala na kumiliki vitu
vilivyokuwa chini ya mwanadamu
1 yohana
3:8
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi
hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili
azivunje kazi za Ibilisi.
Kwa hiyo Dhambi
inapofanyika tu shetani anapata umiliki juu yako,juu ya ardhi yako na juu ya
mipaka yako,ataingia mpaka ndani ya nyumba yako na kumiliki.
Kuna uhusiano kati yako na
mazingira yako na ndio mana unapofanya dhambi wewe katika ulimwengu wa roho
inahesabika kuwa na nchi(ardhi) imefanya Dhambi na kwa hiyo shetani anapata
mlango wa kumiliki ardhi yako.
Ezekiel 14:12
Neno la
BWANA likanijia, kusema, 13Mwanadamu, nchi itakapofanya dhambi na kuniasi, kwa kukosa, nikaunyosha
mkono wangu juu yake, na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuipelekea
njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama;
Kwa hiyo watu wanapofanya dhambi dhambi yao inaathili nchi yao,na kumpa
shetani umiliki.jambo hili humkasirisha Mungu katika namna ambayo ataadhibu
kila mtu na mnyama aliyepo katika hilo eneo
Lakini pia si nchi peke yake bali pia shetani hukamata anga lililopo juu
yako
2 nyakati
7:13
Nikizifunga
mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu
tauni; 14ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na
kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka
mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Unaona athari ya dhambi? Humpa shetani umiliki wa Ardhi hivo ili Mungu
hulazimika kuifunga au kuilaani ardhi na kutokana na kuwa ardhi imekamatwa Anga
nalo hukamatwa na hivo Mungu hulazimika pia kulifunga Anga
Kwahiyo utaona majira yakibadilika katika maisha yako,Mitiririko ya
Kifedha itabadilika,majira ya mvua yatabadilika,na mtililiko maalumu wa mipenyo
ya kimaisha itabadilika
Ona
Mwanzo
3:17
Akamwambia
Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao
nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu
utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo
katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Hiyo mistari
hapo juu inatupa ufahamu zaidi juu ya uhusiano uliopo kati ya mahitaji yako ya
kimwili na Ardhi
Angalia
baada ya adamu kufanya dhambi Mungu hashughuliki kumlani Adamu bali anailaani
ardhi ambayo kwayo alitolewa.
Na matokeo
ya laana hiyo yalileta madhara kwa mwanadamu hata leo.
Kwa hiyo
hivo ndivyo mambo yalivyo.
2. MAAGANO
Hii ni namna
nyingine shetana anapata umiliki wa mipaka na vizazi,kuna idadi kubwa ya watu
ambao wamefanya maagano na shetani kupitia matambiko
Inawezekana
ikawa wewe umeokoka lakini huko uliko toka wanafanya Mambo hayo na kwa hiyo
unakuwa umeunganishwa katika maagano hayo na hivo mipaka yako na umiliki wako
pia unakuwa chini ya Adui
Hautafanikiwa
mpaka umeingia katika ukombozi wa milki na mipaka yako.
Waamuzi 2:2
nanyi
msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu
zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke
mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni
tanzi kwenu.
Wenyeji wa nchi hii ni mapepo ambayo yalitawala Dunia tangia adamu
alipofanya dhambi,kwa hiyo hautakiwi kufanya maagano yoyote nao
Inapotokea ukafanya maagano nayo maandiko yanasema hao mapepo na majini
yatakuwa mwiba katika maendeleo yako.
Hautaenea kokote kule.
MANENO YAKO NA MTAZAMO WAKO JUU YA UMILIKI WAKO
Huu ni mlango mwengine na shetani huutumia sana katika kuhakikisha ya
kuwa hupati milki yako na hata kama umeokoka maandiko yanasema
Mithali
18:21
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake.
Mithali
23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo
vile unavyojiona nafsini
mwako ndivyo ulivyo na ndivyo utakavyokuwa.
JINSI YA KUKOMBOA MILKI YAKO NA MIPAKA YAKO ILI
UWEZE KUIPANUA.
sasa basi
baada ya kuona ni jinsi Gani Shetani amepata umiliki halali wa Mali ambazo hapo
kwanza hazikuwa zake tunaweza kuangalia
sasa ni jinsi Gani ninaweza kukomboa Milki yangu,na kisha nikapanua
mipaka yangu kwa njia ya Maombi
Hapa nataka
ufahamu tu ya Kuwa unaweza ukawa umeokoka lakini unaishi kwenye mazingira au
milki ambayo haijakombolewa na hivyo ukajikuta unashindwa kupanua wigo wako wa
kufanikiwa, kumbuka Nabii yohana katika
1yohana 1:2
Mpenzi, naomba
ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako
ifanikiwavyo.
anasema
mpenzi naomba ufanikiwe na kuwa na afya njema kama roho yako ifanikiwavyo,maana
yake ni kuwa lazima yawepo mahusiano ya ukuaji kati ya roho yako na mazingira
yako ya nje,sasa kama roho yako inakuwa na mazingira yako hayakui basi hapo
kunatatizo ambalo linahitaji kurekebishwa na njia ya kurekebisha ni kama
ifuatavyo.
1.
INGIA KWENYE MAOMBI YA TOBA KWAAJILI
YAKO NA YA ARDHI YAKO
Kuna
uhusiano mkubwa baina yako na Ardhi yako na hapa ninapozungumza juu ya ardhi
ninamaana ya udongo wa eneo unakotokea (Kijijini) na Eneo unalokaa
Nimewahi
kukutana na kesi moja ambayo kwa namna ya kawaida haiwezekani kuitatua,kijana
mmoja ambaye alikuwa akifanya biashara,alihamia kutoka kwao na kuja Dar es
salaam kibiashara,na alipofika akakuta mategemeo yake yamekuwa kinyume,kila
alichokuwa akifanya hakifanikiwi,nilipokutana nae nikamuuliza kama amewahi
kuomba kwaajili ya makazi yake mapya,akaniambia hapana,nikajua tatizo liko
wapi.
Msomaji
nataka ujiulize maswali haya mawili makubwa
1. Kwanini Adamu alipofanya Dhambi Mungu
hakumwadhibu Adamu na badala yake akailaani ardhi mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda
ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;
kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;18michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;19kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo
katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
2. Ukisoma 2nyakati 7:14
Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula
mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, 14kama watu wangu, wanaoitwa kwa jina
langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao
mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi
yao. 15Sasa macho yangu
yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali
hapa.
Mungu anasema ikiwa watu wake
walioitwa Kwa jina lake wakitubu na kuacha dhamb zao Mungu ataponya ardhi yao?
Kuna uhusiano gani hapa kati ya maisha ya Mtu na ardhi
Wakati
unajiuliza swali hilo nataka uunganishe na mstari huu, popote nyayo zenu
zitakapokanyaka hapo nimewapa kuwa milki yenu,kuna uhusiano gani kati ya nyayo
zangu na ardhi yangu
Joshua 1:3
Vipi kama
nyayo zangu zikikanyaga mahali ambapo mamelaaniwa kutokana na makosa ya wenyeji
wa eneo hilo,je nitamiliki kama maandiko yanavyosema?
Mtu wa Mungu
kuna muunganiko wa kiungu wa kumiliki kwako au kufanikiwa kwako kupitia nyayo
zako,
Ardhi hii
unayoikanyaga ndio inayobeba mafanikio yako,kwa kuwa kila unachokiona kwa macho
kimetoka ardhini na aridhini kitarudi
Kwa hiyo
basi ikiwa utaishi mahali ambapo hapo kwanza ardhi yake iliungamanishwa na
maagano ya Kichawi au ulozi jua kabisa yakuwa kama haujapakomboa kupitia maombi
ya Toba si rahis sana wewe kuweza kufanikiwa
Kwa kuwa
wewe utakuwa umekoka sawa,uchawi hauta kusumbua,lakini huo uchawi utakuwa
umebakia katika Ardhi,na hivyo kuzuia kufanikiwa kwako katika eneo hilo.
Utakuwa
ukiomba na kuomba lakini hakuna matokeo,
lakini pia
ikiwa umetoka kwenu maana yake ni kuwa nyayo zako zimebeba Baraka au laana ya
ardhi ya kwenu na ukaja kuishi mahali pengine kama haukujitenganisha na maagano
ya kipepo ya kwenu utasababisha hata ardhi hii mpya kuto kuzalia Matunda
yanayotakiwa
Hivo basi
njia ya kwanza ya kumiliki kwako na kuongezeka kimipaka ni kuingia kwenye
maombi ya Toba kwaajili ya Ardhi yako huku ukiruhusu Damu ya Yesu itembee
kwenye Hiyo Ardhi.
3.
MFUNGE MWENYE NGUVU
Waefeso 6:12
Kwa maana kushindana
kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa
giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho
Katika kila
eneo au mahali kuna mtawala wake wa eneo hili, Ufalme wa shetani umejipanga
vizuri sana na kiakili sana kiasi kuwa kama usipojua kucheza nao utajikuta
unazunguka tu na haupigi hatua yoyote
Wakuu wa
anga ni mapepo au watu ambao wanatawala anga la eneo hilo,hii ina maana kusema
kuwa wameviweka vitu vyote chini yao kama milki yao,hakuna anayeweza kufanikiwa
au kuchomoza bila ruhusa yao
Sasa
unapoingia kwenye eneo ni lazima Baada ya Toba ingia katika kumfunga Mkuu wa
Anga anayetawala katika eneo hilo, kwa kufanya hivo utakuwa umetengeneza njia
ya kufanikiwa kimwili na kimaombi.
4.
VUNJA MADHABAHU ZOTE ZA BAHALI
Ingia katika
maombi ya kuvunja madhabau za Kipepo, kila mahali ambapo kuna ufalme wa kiroho
jua hapo kuna madhabahu za kiroho, kama ni ufalme wa Mungu au ufalme wa giza
Madhabahu ni
eneo ambalo huwa ni kiunganishi cha ulimwengu wa roho kuja mwilini au ulimwengu
wa mwilini kuja rohoni,ni mahali ambapo panaunganisha Mungu na watu wa eneo au
mapepo na watu wa eneo
Katika eneo
kukiwa na madhabahu ya kipepo maana yake watu wanaoishi hapo wameunganishwa na
kufungamanishwa katika madhabahu hizo,sasa kama wewe unataka kumiliki ni lazima
uzivunje madhabahu hizo.
5.
MJENGEE MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA
YAKOBO MADHABAHU
Ukiisha
maliza kuvunja basi mjengee mungu Madhabau, Kama ishara ya kuwaunganisha watu
na Mungu wao, kumbuka ufunuo 5:10 tumefanywa kuwa wafalme na makuhani, kazi ya
kuhani ni hiyo, yaani kuwaunganisha/kuwapatanisha watu na Mungu wao
Kwa hiyo
basi ni Muhimu kujenga madhabahu ya Mungu mahali hapo, ninamaana ya kuwa tenga
eneo au mahali au chumba ambacho kitakuwa madhabahu yako au mnara wa Mungu,
mahali ambapo Mungu atatawala kuanzia hapo mpaka sehemu nyingine za mji.
6.
FANYA MAOMBI YA KUITA NA KUTIISHA
MALI NA UTAJIRI
Hii ni
muhimu sana,kila kitu kina masikio na kina macho,na vitu vyote hutii kwa mwenye
mamlaka ya eneo,hivo basi maombi haya ni maombi ya kuita kwa sauti,ni maombi ya
kutiisha kila kitu katika eneo hilo viite vije kwako iambie Ardhi ikutolee
matunda,iambie ardhi ikuletee watu ,ninaamini baada ya Maombi hayo utaona
upenyo usio wa Kawaida.
7.
LIPE JINA JIPYA ENEO LAKO
Mwanzo 28:18
Yakobo
akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa
chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 19Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo
kwanza uliitwa Luzu.
Tangaza
katika ulimwengu wa Roho,toa jina jipya kulingana na ufunuo ulionao juu ya eneo
lako. Unapo lipa jina eneo maana yake unalivika eneo uwezo flani au nguvu Fulani
kulingana na vile unataka
8.
INUKA ANZA KUMILIKI NA KUTAWALA
Isaya 60:1
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa BWANA umekuzukia
Ninaimani kuwa baada ya somo hili
umetoka hatua kwenda hatua,somo hili ni Muhimu sana ili uweze kufaikiwa,lipo
kwaajili ya kuweka katika matendo ili kuona matokeo
Lakini mwisho kabisa ni muhimu
kufahamu kuwa ufunuo 5:10 inawahusu wale ambao wameokoka tuu,kama haujampokea
Yesu kuwa Mwokozi wako basi fanya hivo leo ili uingie katika jamii ya watawala.
Wasiliana nasi tafadhali au tuma
ujumbe mfupi ukiwa na jina lako na mahali unapotoka ili tuweze kukuombea,.
0763712031
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni